1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madereva wa treni wa Ujerumani wagoma tena leo

12 Machi 2024

Madereva wa treni wa shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn kwa mara nyingine leo hii wanaendelea na mgomo wao wa kushinikiza maslahi bora.

https://p.dw.com/p/4dPWO
Mgomo wa GDL wa Berlin kwenye safari kwa reli
Watu wamesimama kwenye Kituo Kikuu cha Berlin. ilikuwa mgomo wa awali wa masaa 35 wa madereva wa shirika hilo.Picha: Hannes P Albert/dpa/picture alliance

Hatua hiyo ni baada ya hatua ya shirika hilo la kwenda mahakamani kuzuia mgomo huo, kwa kile ilichosema unafayika kinyume cha sheria na hivyo kusubirishwa.

Msemaji wa shirika hilo la reli, amethibitisha kuwa mgomo wa usafirishaji wa abiria unatarajiwa kuanza Asubuhi hii ya Jumanne na unatarajiwa kudumu kwa masaa 24.

Deutsche Bahn imepanga ratiba ya mkutanoo wa dharura kwa lengo  la hata kufanikisha usafirishaji wa japo asilimia 50 ya safari za treni za masafa marefu. Huduma za safari za mji mmoja hadi mwingie na zile za vitongoji nazo pia zimeathirika.

Rufaa hiyo ya shirika la reli Deutsche Bahn haitasikilizwa hadi karibu na adhuhuri ya leo. Na Ikiwa Mahakama ya Kazi ya Jimbo la Hesse itatoa uamuzi tofauti na Mahakama ya Kazi ya Frankfurt, Chama cha Madereva wa Treni GDL kitalazimika kusitisha mgomo wake. Hata hivyo hatua hiyo haimaanishi kurejea kwa mara moja kwa huduma za kawaida usafirishaji.