Maelfu wakimbia mashambulizi kaskazini mwa Msumbiji
28 Februari 2024Matangazo
Hata hivyo, serikali hiyo ilikanusha miito ya hali ya hatari.
Akizungumza na waandishi habari na kuelezea hali ilivyo katika mkoa wa Cabo Delgado, msemaji wa serikali, Filimao Suaze, alisema takribani watu 67,321 wameyakimbia makaazi yao.
Soma zaidi: Msumbiji: Raia sita wauawa kwa kukatwa vichwa na mtawa mmoja auawa kwa kupigwa risasi kichwani
Kwa mujibu wa ripoti za ndani na takwimu za Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), machafuko mapyayalizuka kaskazini mwa Msumbiji wiki mbili zilizopita,
IOM imesema zaidi ya watu 71,681 walikimbia machafuko kati ya Disemba 22 na Februari 25.
Kati ya Jumatano na Alhamisi wiki iliyopita, zaidi ya wakimbizi wapya 30,000 walisajiliwa kuwasili mji wa Namapa kwa mabasi, boti au kwa kutembea.