1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfilipino

Mafuriko yasababisha vifo vya watu 25 nchini Ufilipino

28 Desemba 2022

Idara ya taifa ya kukabiliana na maafa nchini Ufilipino imefahamisha kuwa idadi ya waliofariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko yaliyoshuhudiwa mwishoni mwa juma lililopita imeongezeka hadi watu 25.

https://p.dw.com/p/4LUHE
Philippinen |  Taifun Noru
Picha: Aaron Favila/AP Photo/picture alliance

Karibu watu 400,000 wameathiriwa na mafuriko hayo, huku 9 wakiwa wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 81,000 bado wanapatiwa hifadhi kwenye vituo vya muda.

Vifo 16 kati ya 25 viliripotiwa katika mkoa wa Kaskazini wa Mindanao huku 12 kati ya 26 vimeripotiwa kwenye mkoa wa Mashariki wa Bicol.

Baraza la usimamizi wa maafa limesema kuwa nyumba 1,196 ziliharibiwa na mafuriko, huku sehemu 123 za barabara na madaraja 12 vikiathirika.

Baadhi ya maeneo yamesalia bila huduma ya umeme au maji safi. Kila mwaka takriban vimbunga 20 pamoja na dhoruba huikumba Ufilipino, moja ya nchi zinazokumbwa na maafa zaidi duniani.