1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Magenge ya wahalifu yaanzisha mashambulizi mapya Haiti

22 Aprili 2024

Magenge yenye silaha yameanzisha mashambulizi mapya katika sehemu kadhaa za mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4f288
Vurugu za magenge ya uhalifu nchini Haiti
Kifaru kidogo cha Polisi kikifanya doria katika mji mkuu wa Haiti Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Hayo yanajiri wakati taifa hilo la Carribean likijiandaa kuidhinishwa kwa Baraza la mpito lenye wajumbe tisa ambao jukumu lao ni kuunda serikali mpya.

Milio ya risasi na miripuko vilisikika karibu na Ikulu na katikati mwa jiji katika eneo la Lower Delmas lililogeuka kuwa uwanja wa vita kati ya polisi na magenge ya wahalifu ambayo yanadhibiti karibu asilimia 90 ya mji mkuu wa Haiti.

Soma pia: Umoja wa Mataifa wasema idadi ya vifo yaongezeka Haiti

Kufuatia shinikizo la Marekani, Waziri Mkuu Ariel Henry aliahidi kujiuzulu mnamo Machi 11 lakini taifa hilo limeendelea kushuhudia vurugu za magenge hayo. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu 360,000 wa Haiti wamekuwa wakimbizi wa ndani huku mamilioni ya wengine wakikabiliwa na njaa.