Mahakama Pakistan yampa dhamana Nawaz Sharif
19 Oktoba 2023Uamuzi huo wa mahakama unamruhusu kurejea katika mji wake wa Lahore siku ya Jumamosi (Oktoba 21), kwa ajili ya mkutano wa kumkaribisha nyumbani ulioandaliwa na chama chake, wakati mpinzani wake mkuu, Imran Khan, akisota gerezani.
Soma zaidi: Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aondolewa madarakani
Wakili wake, Amjad Pervaiz, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mahakama imempatia mteja wake dhamana ya ulinzi hadi Oktoba 24 na kuongeza kuwa hawezi kukamatwa atapowasili akitokea nchini Uingereza kwa matibabu.
Soma zaidi: Sharif achaguliwa waziri mkuu mpya Pakistan baada ya kuondolewa Khan
Sharif alihudumu kama waziri mkuu katika awamu tatu tafauti na aliondolewa 2017, na kuzuiliwa kujihusisha na siasa maisha yake yote baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.