1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama EAC yakataa pingamizi la mradi wa bomba la mafuta

30 Novemba 2023

Mahakama ya kikanda imetupilia mbali pingamizi la kisheria kuhusu mradi wa bomba la mafuta wa mabilioni ya dola nchini Tanzania na Uganda ambao umekosolewa vikali na wanaharakati wa mazingira na wale wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/4ZcAL
Nigeria Umwelt l Undichte Ölleitungen verseucht das Land im Nigerdelta
Picha: Friedrich Stark/imago

Mahakama ya kikanda imetupilia mbali pingamizi la kisheria kuhusu mradi wa bomba la mafuta wa mabilioni ya dola nchini Tanzania na Uganda ambao umekosolewa vikali na wanaharakati wa mazingira na wale wa haki za binadamu.

Soma pia:Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba 
     
Jopo la Majaji watano wa Mahakama ya Afrika Mashariki yenye makao yake jijini Arusha, wametoa uamuzi hapo jana kwamba haikuwa na mamlaka ya kusikiliza pingamizi lililowekwa na mashirika kadhaa ya kiraia kwa sababu liliwasilishwa  kuchelewa.
      
Bomba hilo ni sehemu ya mradi wa dola bilioni 10 unaoongozwa na kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa ya TotalEnergies ambao unalenga kuendeleza vyanzo vya nishati hiyo huko Uganda na kusafirisha mafuta ghafi hadi Tanzania kwa mauzo ya nje.