Mahakama ya Katiba Afrika Kusini yampiga Stop Zuma
20 Mei 2024Mahakama ya juu nchini Afrika Kusini imetoa uamuzi wake leo Jumatatu wa kumpiga marufuku rais wa zamani Jacob Zuma kugombea katika uchaguzi wa bunge utakaofnyika wiki ijayo kwa sababu kwamba alipatikana na hatia ya kuidharau Mahakama mwaka 2021 na hilo ndilo lililodhibiti ushiriki wake katika uchaguzi huo.
Soma pia: Zuma hastahili kugombea katika uchaguzi mkuu Afrika Kusini
Korti ya katiba iliamua kuwa kufuatia Zuma kupewa kifungo cha miezi zaidi ya12 jela kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake ya tuhuma za kuhusika na rushwa imemfanya kutokuwa na uhalali wa kushiriki uchaguzi huo.
Mwezi wa Januari chama chake cha zamani ambacho ndio chama tawala cha African National Congress ANC killisimamisha uanachama wa Zuma aliye na miaka 82. Na tangu wakati huo aliunda chama chake cha Umkhonto we Sizwe (MK) na alitarajia kusimama kama mwenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi wa May 29.