SiasaMarekani
Mahakama ya rufaa: Trump hana kinga ya kutoshtakiwa
7 Februari 2024Matangazo
Uamuzi huo wa kihistoria umetolewa mjini Washington na Majaji watatu wa Mahakama ya rufaa ya shirikisho.
Majaji hao wamesema hoja ya Trump ya kwamba anayo kinga ya kutoshtakiwa kwa hatua zote alizozichukua akiwa kama rais, haina mashiko na kwamba inakinzana na historia, misingi ya katiba ya Marekani na kwamba hatua kama hiyo ingedhoofisha mfumo wa mihimili mitatu ya uongozi.
Muda mfupi baada ya uamuzi huo, msemaji wa timu ya kampeni ya Trump , Steven Cheung amesema rais huyo wa zamani "hakubaliani kabisa na uamuzi huo na kwamba atakata rufaa katika Mahakama ya Juu ya Marekani.