Mahmoud Abbas ataja kuwa tayari kuiongoza Gaza baada ya vita
18 Januari 2025Katika taarifa yake ya kwanza tangu kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, Mahmoud Abbas amesema serikali yake imekamilisha maandalizi yote ya kuwajibika kikamilifu huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuwarejesha waliokimbia makazi yao, kutoa huduma za msingi, usimamizi wa vivuko na ujenzi wa eneo lililoharibiwa na vita.
Kundi la Hamas ambalo limekuwa na udhibiti kamili huko Gaza tangu mwaka 2007 baada ya kushinda uchaguzi wa bunge mwaka 2006, limesema halihitaji kuitawala tena Gaza baada ya mzozo huo.
Soma pia:Mahmoud Abbas: Acheni kuipatia Israel silaha
Mpinzani wake ambaye ni vuguvugu la Fatah, linaongoza serikali inayofahamika kama Mamlaka ya Palestina na kusimamia eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu. Hata hivyo Israel imekuwa ikipinga uongozi wa makundi hayo huko Gaza baada kumalizika kwa mzozo huo.