Maji Smarti ni mfumo wa kielektroniki unaowezesha kutoa taarifa za kiwango cha maji kilichopo katika chanzo husika, pamoja na kugundua kama kuna uharibifu wa miundombinu ya maji. Mfumo huu umetengenezwa na wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari ya Arusha Sayansi, iliyoko kaskazini mwa Tanzania. Mfumo huo tayari umeanza kutumika katika shule hiyo.