Mali, Niger kujiondowa kwenye makubaliano na Ufaransa
6 Desemba 2023Matangazo
Hii ni hatua nyingine ya kusambaratisha uhusiano na mkoloni huyo wa zamani, huku mataifa hayo jirani yakiimarisha mahusiano yao.
Katika taarifa ya pamoja, mataifa hayo ya Afrika Magharibi yamesema bado kunashuhudiwa "hali ya uhasama wa Ufaransa" dhidi ya mataifa yao na kusisitiza kuwa mikataba hiyo haina usawa na inasababisha hasara kubwa ya mapato kwa Mali na Niger.
Soma zaidi: Balozi wa Ufaransa aondoka Niger
Haikuwa wazi mara moja ni zipi athari za kiutendaji kufuatia uamuzi huo.
Ufaransa imekuwa na makubaliano ya ushuru na mataifa hayo kwa miaka mingi ambayo yanahusisha kodi ya mapato, ushuru wa urithi na ule wa usajili.
Mikataba hiyo inalenga kukuza ushirikiano katika masuala ya kifedha.