Marekani, Korea Kusini zakanusha kuingia Korea Kaskazini
11 Julai 2023Hayo yanajiri baada ya dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yo Jong, ambaye pia ni mmoja wa maafisa wakuu wa sera za kigeni wa kaka yake, Kim Jong Un, kudai kuwa ndege za kivita za nchi hiyo zilipambana kuifurusha ndege ya Marekani.
Soma zaidi: Japan itaharibu kombora litakalorushwa na Korea Kaskazini
Mapema jana, Wizara ya Ulinzi ya Korea Kaskazini iliishutumu Marekani kwa kurusha mara kadhaa ndege za upelelezi na za kimkakati katika anga lake na kuonya kwamba ndege zitakazokiuka mamlaka yake zinaweza kudunguliwa.
Soma zaidi: Korea Kaskazini: Ushirika wa Korea Kusini na Marekani utachochea uhasama
Hata hivyo, Marekani imeitolea wito Korea Kaskazini kujiepusha na kile ilichokiita kuwa ni "harakati za kuchochea mvutano" na badala yake "ishiriki katika diplomasia iliyo thabiti."