Marekani na Vietnam zaazimia kujenga 'ushirika wa kimkakati'
15 Aprili 2023Marekani na Vietnam zimesema zinayo matumaini ya kuimarisha mahusiano yao ya kidiplomasia na kuyaweka katika kiwango cha ''washirika wa kimkakati.''
Hayo yametangazwa baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, aliyepita nchini Taiwan akielekea Japan kushiriki katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi zilizoendelea kiviwanda la G7.
Kwa miaka 10 iliyopita, Vietnam na Marekani zimekuwa zikishirikiana zaidi kibiashara, huku zote zikitazama kwa wasiwasi mkubwa kuongezeka kwa nguvu za kijeshi za China katika ukanda wa Bahari ya China Kusini.
Hata hivyo, watafiti wanasema Vietnam inasitasita kusogeleana zaidi na Marekani kwa hofu ya kuikasirisha China, licha ya kuwepo mzozo wa kimpaka baina ya Vietnam na China katika bahari ya China Kusini. China ambayo ni jirani wa Vietnam upande wa kaskazini pia ni mshirika mkuu wa nchi hiyo kibiashara.
Chanzo: AFPE