SiasaMarekani
Marekani yasimamisha misaada ya chakula nchini Ethiopia
8 Juni 2023Matangazo
Msemaji wa shirika hilo ameeleza katika taarifa, kwamba USAID na serikali ya Ethiopia wamegundua kuwapo kwa hila iliyoratibiwa, ya kuubadishia njia msaada wa chakula ili usiwafikie wenye mahitaji. Ingawa msemaji huyo hakuwataja wahusika, nyaraka za muungano wa mashirika ya msaada zinawatuhumu maafisa wa tawala za mikoa na vikosi vya jeshi kujinufaisha na msaada huo.
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa kabisa wa Ethiopia katika sekta ya msaada wa kibinadamu, ambapo inawasaidia watu wapatao milioni 20 wanaokumbwa na njaa kutokana na ukame na pia vita katika jimbo la Tigray ambavyo vilimalizika hivi karibuni.