SiasaHaiti
Marekani yatangaza msaada mpya wa dola milioni 160 kwa Haiti
26 Septemba 2024Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye alifanya ziara katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mapema mwezi huu ametoa tangazo hilo pembezoni mwa mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille , rais wa baraza la mpito Edgard Leblanc Fils, pamoja na mawaziri kutoka Kenya, Canada, Ufaransa, na wanachama wa Jumuiya ya nchi za Caribbean (Caricom).
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, msaada huo utatumiwa kwenye sekta ya maendeleo, uchumi, afya na usalama kwa watu wa Haiti, na hivyo kupelekea msaada wa Marekani kwa nchi hiyo ya Caribbean kufikia hadi dola bilioni 1.3 tangu mwaka 2021.