UgaidiAfrika
Marekani yawawekea vikwazo viongozi wa makundi ya kigaidi
24 Aprili 2024Matangazo
Vikwazo hivyo viliwalenga viongozi wa tawi la kundi la kigaidi la al-Qaeda huko Afrika Magharibi liitwalo Jama'at Nusrat al-Islam wal Muslimeen (JNIM), pamoja na Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Mourabitoun.
Kwa miaka kadhaa sasa, nchi za Afrika Magharibi zimekuwa zikikabiliwa na uasi wa makundi yenye itikadi kali za Kiislamu ambayo yalikita mizizi nchini Mali mnamo mwaka 2012, na kutanua udhibiti wao katika eneo la Sahel licha ya juhudi za kijeshi zinazoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.