Mashambulizi ya Urusi yaua sita Ukraine
1 Oktoba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine, mashambulizi hayo yalifanyika asubuhi ya Jumanne (Oktoba 1), wakati raia kote nchini humo walikuwa wakitowa heshima zao kwa wanajeshi na watu waliouwawa kwenye vita vinavyoendelea kwa kukaa kimya kwa dakika moja.
Soma zaidi: Watu saba wauawa kwa shambulizi la Urusi nchini Ukraine
Gavana wa eneo hilo, Oleksandar Prokudin, alichapisha video iliyoonesha miili ya watu waliouwawa ikiwa imelala karibu na maduka ikiwa imefunikwa na nyanya na mboga mboga.
Taarifa pia zinasema Urusi iliwakamata watu kiasi 39 iliyowaita wafuasi wa makundi ya kigaidi ya Ukraine.