Mataifa ya Baltic NATO yajadili usalama mkutano wa Helsinki
14 Januari 2025Katika matukio ya karibuni, nyaya kadhaa za umeme na za intaneti zinazopita chini ya Bahari ya Baltic zilidaiwa kukatwa makusudi.
Madhumuni kuu ya mkutano huo ni kutafuta njia za kulinda vyema miundombinu muhimu katika Bahari ya Baltic na kukabiliana na tishio la kile kinachoitwa meli za kivuli za Kirusi ambazo husafiri kisirisiri.
Soma pia: NATO, Urusi wafanya luteka mkabala bahari ya Baltiki
Hii inahusu meli ambazo Urusi hutumia kusafirisha mafuta, kwa mfano, ili kukwepa vikwazo vilivyowekwa kutokana na uvamizi wake wa Ukraine.
Mkutano huo unaongozwa na Rais wa Finland Alexander Stubb na Waziri Mkuu wa Estonia Kristen Michal. Viongozi wa nchi za NATO katika eneo la Baltic pia wanatarajiwa kuhudhuria, zikiwemo Denmark, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Poland na Sweden. Mkuu wa NATO, Mark Rutte, pia atahudhuria.