1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kuijadili Niger

31 Agosti 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo nchini Uhispania kujadili juu ya kadhia nchini Niger - ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuiwekea nchi hiyo vikwazo.

https://p.dw.com/p/4VmGK
Baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika picha ya pamoja mjini Brussels
Baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika picha ya pamoja mjini BrusselsPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Mawaziri hao wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia wameeleza kufuatilia juu ya kinachoendelea Gabon baada ya jeshi kutangaza kutwaa madaraka.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amewaambia waandishi wa habari kuwa, mapinduzi nchini Niger yamefungua enzi mpya ya kukosekana kwa utulivu katika ukanda wa Sahel ambao tayari unakumbwa na uasi.

Kukosekana kwa utulivu katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, na vita vya nchini Ukraine ni baadhi ya ajenda watakazozijadili kwenye mkutano wao mjini Toledo.

Hassoumi Massoudou, waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Niger iliyoondolewa madarakani na Omar Touray, mkuu wa tume ya ECOWAS pia watahudhuria mkutano huo.