1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiMexico

Mawaziri wa Marekani na Mexico kujadili wimbi la wahamiaji

27 Desemba 2023

Mawaziri wawili wa Marekani wanakwenda nchini Mexico leo kukutana na rais Manuel Lopez Obrador kwa mazungumzo juu ya wimbi ya wahamiaji kutoka Amerika ya Kati wanaopitia Mexico kujaribu kuingia Marekani.

https://p.dw.com/p/4abEy
Mexico Tapachula 2023 | Msafara wa wahamiaji na waomba hifadhi
Msafara wa wahamiaji na waomba hifadhi wengi kutoka nchini kadhaa za Amerika ya Kati wakikatisha Mexico njiani kwenda mpaka wa Marekani.Picha: Edgar H. Clemente/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni, Antony Blinken, na mwenzake wa Mambo ya Ndani, Alejandro Mayorkas, watajadiliana na rais Obrador namna Marekani na Mexico zinavyoweza kufanya kazi pamoja kutatua changamoto za usalama mipakani.

Mkutano huo utafanyika ikiwa ni wiki moja tangu rais Obrador alipozungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani, Joe Biden, na kukubaliana kwamba mifumo zaidi ya ulinzi na usalama inahitajika kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Hivi sasa kundi kubwa la wahamiaji na waomba hifadhi kutoka nchi kadhaa za Amerika ya Katiambalo liliingia ndani ya ardhi ya Mexico siku kadhaa zilizopita, linaendelea na safari kwa malengo ya kuufikia mpaka wa Marekani.