1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kutafuta amani Sudan ya kwama

8 Novemba 2023

Saudi Arabia imesema pande zinazohasimiana nchini Sudan hazijapiga hatua yoyote kuelekea kufikia makubaliano ya usitishwaji wa mapigano katika mazungumzo yao ya sasa.

https://p.dw.com/p/4YYH7
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan akiwa na wajumbe wa pande zinazozozana Sudan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan akiwa na wajumbe wa pande zinazozozana Sudan.Picha: AFP

Saudi Arabia imesema, badala yake zimesisitiza kuheshimiwa mikataba iliyopita kuimarisha upatikanaji na upelekaji wa misaada ya kibinaadamu. 

Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limeripoti kwamba mwenyeji wa mazungumzo hayo, Saudi Arabia inasikitika kwamba pande hizo mbili zimeshindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano wakati wa duru hii ya kwanza, kwa kuwa hakuna suluhisho la kijeshi linalokubalika kwa mzozo wa Sudan. 

Soma pia:Mauaji ya kikabila yaripotiwa kuongezeka Darfur Magharibi

Haikubainika baada ya mazungumzo ya jana ni hatua zipi zitakazofuata.

Pande mbili zinazozozana Sudan zimekubaliana kushirikiana na Umoja wa Mataifa kushughulikia vizuizi vya upelekaji wa misaada ya kibinadamu na kutambua vituo vya mawasiliano ili kuratibu safari za wafanyakazi wa mashirika ya utoaji misaada.