1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjane wa Navalny aahidi kuendeleza kazi yake

19 Februari 2024

Mjane wa kiongozi wa upinzani wa Urusi, Alexei Navalny, Yulia Navalnaya, ameapa kuwa ataendelea na kazi yake ya kupambania uhuru wa nchi yake huku akitoa wito kwa wafuasi wake kuendelea kumuunga mkono.

https://p.dw.com/p/4caOi
Umoja wa Ulaya | Yulia Nawalny na Josep Borrell
Mjane wa Alexei Navalny akiteta na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell Picha: FRANCOIS LENOIR/European Union

Navalnaya, ambaye amewasili hii leo mjini Brussels na kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya, amesema katika video kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin ndiye aliyemuua mumewe, ambaye alifariki siku ya Ijumaa akiwa gerezani.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema yeyote aliyehusika na kifo cha Alexei Navalny atawajibishwa.

" Bila shaka nchi wanachama zitapendekeza vikwazo dhidi ya mhusika aliyetenda hilo. Mhusika mkuu ni Putin mwenyewe. Lakini tunaweza kuangazia zaidi muundo na mfumo wa taasisi za jela nchini Urusi. Lakini tusisahau ni nani hasa anayehusika kwa kifo hiki cha Navalny," alisema Borrell.

Soma pia:

Ikulu ya Kremlin imesema hii leo kuwa uchunguzi kuhusu kifo cha Navalny unaendelea, huku ikilaani kauli za mataifa ya Magharibi ambazo zinadai kuwa Putin ndiye anayehusika na kifo cha mpinzani huyo.