1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuMarekani

Mke wa 'El Chapo" aachiwa huru kutoka jela nchini Marekani

14 Septemba 2023

Mke wa mlanguzi maarufu wa dawa za kulevya kutoka Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman, ameachiwa huru jana Jumatano baada ya kukaa jela kwa takriban miaka miwili.

https://p.dw.com/p/4WJHD
Emma Coronel Aispuro
Picha: Jesse Ward/New York Daily News/TNS Photo/Newscom/picture alliance

Emma Coronel Aispuro aliyekamatwa na Polisi mwaka 2021, alihukumiwa baada ya kuhusishwa na makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Malkia huyo wa zamani wa urembo mwenye umri wa miaka 34 na aliyeolewa na El Chapo akiwa hajatimiza miaka 18, alihukumiwa Novemba mwaka 2021 kifungo cha miaka mitatu jela.

Soma pia: El-Chapo afungwa maisha

USA | Ankunft von El Chapo nach seiner Auslieferung an die USA
El Chapo Guzman (Katikati) akiwasili nchini Marekani mwaka 2017Picha: U.S. law enforcement/AP/picture alliance

Wakati wa kesi yake, waendesha mashtaka na mawakili wake wa utetezi walisema Coronel hakuhusika katika biashara haramu ya Guzman ambapo genge lake la uhalifu la "Sinaloa Cartel", lilisafirisha nchini Marekani mamia ya tani za dawa za kulevya aina ya kokeini na heroini.

Guzman alihamishwa kutoka Mexico hadi Marekani mwaka 2017 na kuhukumiwa Julai 2019 kifungo cha maisha jela.