Mpango wa Chakula, WFP waomba utulivu nchini Sudan
28 Oktoba 2024Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP limetoa wito huo wakati nchi hiyo ikikabiliwa na uwezekano mkubwa wa kutumbukia kwenye baa la njaa.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Cindy McCain, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanataka nafasi ya kuingia kikamilifu nchini humo pamoja na kuwa na uwezo wa kufikia vituo vingi kadri inavyowezekana, ndani ya nchi hiyo.
Pande zote kwenye mzozo wa Sudan zimetuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwalenga raia na kuzuia msaada kuwafikia wale wanaohitaji, sambamba na kutumia mbinu zinazosababisha mamilioni ya watu kukosa chakula.
McCain ameonya kwamba nchi nzima hivi sasa inakabiliwa na kitisho cha njaa na tayari baa la njaa limeshatangazwa katika kambi wa wakimbizi wa ZamZam kwenye jimbo la Darfur.