MigogoroSudan
Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa Sudan
16 Oktoba 2024Matangazo
Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan anayehusika na masuala ya wakimbizi Mamadou Dian Balde, amesema idadi hiyo ya watu milioni tatu huenda ikaongezeka maradufu ndani ya wiki mbili hadi tatu zijazo, na kusisitiza kuwa janga hilo linalohusishwa moja kwa moja na kuongezeka kwa ukatili katika mzozo huo.
Vita hivyo vilivyoanza mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la Sudan likiongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na vikosi vya Msaada wa Haraka vya RSF vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.