MigogoroSudan
Jeshi la Sudan laua watu 23 kwenye soko kuu mjini Khartoum
13 Oktoba 2024Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa Jumapili na mtandao wa vikosi vya waokoaji wa kujitolea nchini humo ambao umesema kuwa majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Vita kati ya jeshi la nchi hiyo na kundi la RSF vimeitumbukiza Sudan katika hali mbaya zaidi ya kibinaadamu huku kukiwa na mamia ya vifo na mamilioni ya watu wakilazimika kuyahama makazi yao.
Soma pia: Watu wa Sudan wanakabiliwa na hali ya kutisha
Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha pia ongezeko kubwa la utapiamlo na njaa. Shirika la kutoa misaada la Madaktari wasio na Mipaka la MSF limesema watu milioni 26 ikiwa ni karibu nusu ya idadi jumla ya watu wa Sudan, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.