Mpango usitishwaji mapigano kati ya Israel-Hamas watekelezwa
24 Novemba 2023Kundi la kwanza la mateka 13 ambao ni wanawake na watoto wanaoshikiliwa na Hamas wanatarajiwa kuachiwa huru baadae leo, huku Israel nayo ikiwaachia wafungwa Wakipalestina wapatao 150.
Malori ya mafuta yamefanikiwa pia kuingia Gaza kupitia kivuko cha mpakani cha Rafah.
Awali, Misri ilisema lita 130,000 za dizeli, lori nne za gesi na malori 400 ya misaada ingelisafirishwa kila siku hadi Gaza.
Soma pia:Usitishwaji mapigano kuanza Gaza, mateka kuachiwa
Makubaliano hayo yanaleta ahueni kwa wakaazi milioni 2.4 wa Gaza ambao wamekuwa wakikabiliwa na wiki saba za mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel baada ya shambulizi la Hamasla Oktoba 7 ambalo Israel inasema watu 1,200 waliuawa.
Nayo mamlaka ya Hamas, imesema hadi sasa tayari watu 15,000 wameuawa.