1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

MSF yawataka wapiganaji Kongo kutozishambulia hospitali

9 Machi 2024

Shirika la Kimataifa la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limeelezea kushtushwa na shambulizi dhidi ya hospitali moja Mashariki mwa Kongo na kuzitaka pande zinazozozana kuwalinda raia na taasisi za matibabu

https://p.dw.com/p/4dL12
Ujumbe wa MONUSCO wawasili katika kambi ya Rho nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
Ujumbe wa MONUSCO wawasili katika kambi ya Rho nchini jamhuri ya kidemokrasi ya KongoPicha: Paul Lorgerie/DW

MSF imesema kuwa wanaume waliokuwa wamejihami kwa silaha, walishambulia mji wa Drodro katika jimbo la Ituri usiku wa Machi 6 na 7 na kumuuwa mgonjwa mmoja mzee aliyekuwa amelala kitandani na pia kuiba vifaa vya matibabu.

Soma pia:Watu 15 wameuawa na maelfu wamekimbia mashambulizi ya waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Maelfu ya watu wametafuta hifadhi umbali wa kilomita 10 kutoka kambi ya watu wanaoishi na ulemavu ya Rho, iliyojengwa kutoa hifadhi kwa watu wasiozidi 30,000 lakini kwasasa ina watu mara mbili zaidi ya idadi hiyo.

Soma pia:Wakaazi mashariki mwa Congo wakabiliwa na uhaba wa chakula

MSF imewaondoa kwa muda wafanyakazi wake kutoka Drodro, na wakati ikiendelea kutoa huduma ya matibabu kwa watu hao katika kambi ya Rho, imesema hatua hiyo sio endelevu.

Meneja wa mpango wa MSF kwa Kongo Stephanie Giandonato, amesema kilichotokea katika eneo hilo ni  jambo la kutia hofu.