MigogoroUkraine
Mtu mmoja auwawa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine
26 Septemba 2024Matangazo
Jeshi la anga la Ukraine limesema vikosi vya Urusi vilifanya mashambulizi 78 ya droni na makombora sita katika maeneo mbalimbali kote nchini wakati wa shambulizi lililodumu kwa muda wa masaa kadhaa.
Jeshi pia limesema mifumo ya ulinzi wa makombora umeziharibu droni 66 na makombora manne.
Soma pia: Zelensky asema hakuna mazugumzo ya amani ya Urusi
Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Ihor Klymenko, ameandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba mwanamke mmoja ameuwawa katika shambulizi la kombora huko Odesa kusini mwa Ukraine na watu wengine wanane wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu kwenye mji wa Zaporizhzhia, kusini mashariki mwa nchi.
Droni kadhaa zimeharibiwa katika anga la mji mkuu Kiev ambako magari 20 na bomba la gesi limeharibiwa.