Muungano wa upinzani wafanikiwa wingi wa viti Poland
17 Oktoba 2023Matangazo
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yaliyotangazwa leo mjini Warsaw yamethibitisha kwamba chama cha PiS cha Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki kimeshinda kwa kujikingia asilimia 35.38 ya kura huku chama cha upinzani cha kiliberali cha Civic Coalition cha waziri mkuu wa zamani, Donald Tusk, kikifuata katika nafasi ya pili na asilimia 30.7 ya kura.
Soma zaidi: Tusk aibuka mshindi uchaguzi Poland
Matumaini ya EU baada ya uchaguzi wa Poland
Hata hivyo, muungano wa Tusk una njia rahisi ya kuunda serikali ya mseto na chama cha kihafidhina cha Third Way ambacho kimepata asilimia 14.4 ya kura na chama cha siasa za mrengo wa kushoto The Left ambacho kimeshindia asilimia 8.61 ya kura.
Muungano huu utakuwa na wingi wa viti 248 kati ya viti 460 bungeni.