SiasaUfaransa
Mwanahabari wa Ufaransa aliyetekwa 2021 aachiwa huru Mali
21 Machi 2023Matangazo
Mwanahabari huyo pamoja na mfanyakazi wa misaada wa Kimarekani aliyeshikiliwa pia mateka na wanamgambo hao kwa miaka sita waliwasili jana mjini Niamey baada ya kuwachiwa huru.
Mfaransa Olivier Dubois na Mmarekani Jeffery Woodke waliwasili kwa ndege jana katika uwanja wa Niamey, mji mkuu wa Niger. Dubois mwenye umri wa miaka 48 alitekwa nyara nchini Mali mnamo Aprili 2021 wakati Woodke alitoweka nchini Niger mnamo Oktoba 2016.
Soma pia: Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu waliotekwa Mali, waachiwa huru
Wawili hao walizishukuru serikali za Niger, Ufaransa na Marekani kwa kushughulikia kuwachiliwa kwao. Maelezo kuhusu ni kwa nini na vipi wawili hao waliwachiwa huru hayakutolewa.