SiasaUkraine
NATO kuzisaidia nchi wanachama kununua makombora ya Patriot
3 Januari 2024Matangazo
NATO imeongeza kuwa utengenezaji wa makombora barani Ulaya utapanuliwa, hii ikiwa ni kufikia azma ya ulinzi inayofahamika kama "Mpango wa Ngao ya Ulaya,"- ESSI.
Hayo yakijiri, vita katika bara la Ulaya vimeendelea kupamba moto ambapo Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana huku Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ikisema kuwa mkururo wa hivi karibuni wa mashambulizi ya Moscow umekuwa ukiyalenga maeneo ya kijeshi badala ya miundombinu ya nishati kama ilivyokuwa mwaka jana wakati wa majira ya baridi.
Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmygal amesema Kyiv inategemea msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wake wa Magharibi, huku akikadiria kuwa mwaka huu, nchi hiyo itahitaji karibu dola bilioni 37.