NATO yamteua Mark Rutte kuwa Katibu Mkuu wake ajae
26 Juni 2024Matangazo
Uteuzi huo unamuweka Waziri Mkuu huyo wa Uholanzi anayemaliza muda wake kushikilia wadhifa wa moja ya mashirika makubwa ya kiusalama duniani katikati ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Uteuzi wa Rutte umeidhinishwa na mabalozi wa NATO wakati wa mkutano uliofanyika mjini Brussels wa jumuiya hiyo ya kujihami yenye nchi wanachama 32.
Orban asema yuko tayari kuunga mkono azma ya Mark Rutte NATO
Rais wa Marekani Joe Biden na wenzake watamkaribisha rasmi Mark Rutte katika mkutano wa kilele mjini Washington mnamo Julai 9 hadi 11.
Rutte atachukua nafasi ya katibu mkuu wa sasa Jens Stoltenberg kuanzia Oktoba mosi.