Navalny kuzikwa Moscow
1 Machi 2024Matangazo
Ilitarajiwa kungekuwepo idadi kubwa ya polisi wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika mchana wa Ijumaa katika makaburi ya Borisov baada ya ibada kanisani.
Kulikuwa na hofu kwamba maafisa wa polisi wangeliwazuia baadhi ya waombolezaji.
Soma zaidi: Navalny atarajiwa kuzikwa kusini mwa jiji la Moscow
Hivi karibuni mamia ya watu walikamatwa na polisi kwa kuweka mashada ya maua kumuomboleza Navalny.
Kulingana na taarifa rasmi ya serikali, Navalny aliyekuwa na umri wa miaka 47, na pia mkosoaji mkubwa wa Rais Vladimir Putin, alikufa Februari 16 akiwa gerezani.
Mjane wake, Yulia Navalnaya, na timu yake ya wanaharakati, walimtuhumu Rais Putin kwa kumuua mwanasiasa huyo.