SiasaSierra Leone
Rais wa zamani wa Sierra Leone ashtakiwa kwa uhaini
4 Januari 2024Matangazo
Rais huyo Ernest Bai Koroma anadaiwa kujihusisha na kile ambacho serikali ilikiita jaribio la mapinduzi la mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Koroma aliyekuwa rais kati ya mwaka 2007 na 2018 alihojiwa na polisi mara tatu kabla ya kufunguliwa mashtaka.
Anahusishwa na mashambulizi ya silaha katika kambi kubwa ya jeshi nchini humo pamoja na gereza lenye ulinzi mkali lililopo kwenye mji mkuu, Freetown Novemba 26.
Karibu wafungwa 2,000 walitoroka katika shambulizi hilo, miongoni mwao wakiwa ni watuhumiwa waliohusishwa na mapinduzi hayo.
Zaidi ya watu 50 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na binti wa Koroma.