Rais wa zamani atuhumiwa jaribio la mapinduzi Sierra Leone
13 Desemba 2023Matangazo
Mkuu wa polisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi, Fayia Sellu, amesema kwa mujibu wa maelezo aliyoandikisha kwa hiyari yake, Koroma anatuhumiwa kushiriki jaribio hilo.
Jumamosi iliyopita, mamlaka nchini Sierra Leone zilisema rais huyo wa zamani alikuwa kwenye kizuizi cha nyumbani wakati akifanyiwa mahojiano.
Soma zaidi: Aliyepanga mapinduzi Sierra Leone akamatwa
Siku ya Jumanne (Disemba 12), serikali kupitia waziri wake wa habari, Chernor Bah, ilithibitisha kuwa sasa Koroma ni mtuhumiwa rasmi.
Kundi la watu wenye silaha lilivamia ghala la silaha la jeshi, kambi mbili, jela mbili na vituo viwili vya polisi mapema ya tarehe 26 Novemba, ambapo kwenye makabiliano na vyombo vya usalama, watu 21 waliuawa.