MigogoroMashariki ya Kati
Netanyahu aafiki kuanzishwa duru mpya ya mazungumzo
30 Machi 2024Matangazo
Hatua hii inajiri siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, kuiamuru Israel kuhakikisha misaada ya kiutu inawafikia raia.
Ofisi ya Netanyahu imesema mazungumzo hayo mapya yatafanyika siku zijazo katika nchi za Qatar na Misri, huku kukiwa na miongozo iliyo tayari ili kusaidia kufanikisha mazungumzo ambayo yalionekana kukwama katika siku za hivi karibuni.
Soma pia: Netanyahu akubali kupeleka wajumbe wa Israel Misri na Qatar
Licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapema wiki hii lililoamuru "kusitishwa mara moja kwa mapigano", mashambulizi kadhaa yaliripotiwa huko Gaza usiku wa kuamkia Jumamosi. Wizara ya afya huko Gaza imesema makumi ya watu wameuawa wakiwemo watu 12 huko Rafah.