1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Pande hasimu Sudan zatakiwa kuruhusu misaada kuwafikia raia

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2024

Nchi za Magharibi zikiwemo Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ujerumani siku ya Ijumaa zimezitolea mwito pande mbili katika vita vya Sudan kuruhusu usambazaji wa misaada.

https://p.dw.com/p/4lyj2
Mtawala mkuu wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan
Mtawala mkuu wa Sudan Abdel Fattah al-BurhanPicha: Sudanesischer Übergangsrat/XinHua/dpa/picture alliance

Nchi za Magharibi zikiwemo Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ujerumani siku ya Ijumaa zimezitolea mwito pande mbili katika vita vya Sudan kuruhusu usambazaji wa misaada inayohitajika haraka kwa mamilioni ya watu.

Katika taarifa ya pamoja mataifa hayo yametaka kuondolewa kwa vizuizi katika mpaka wa Adre unaoingia Chad, ambapo Umoja wa Mataifa unasema malori yake yanasubiri vizuizi viondoshwe.

Soma: Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa Sudan

Vita vilipamba moto nchini humo tangu Aprili mwaka 2023 kati ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) chini ya mtawala mkuu wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan na Kikosi cha wanamgambo (RSF), kinachoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo. Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita. Mzozo huo umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu zaidi ya watu milioni 11 kukimbia makazi yao.