Papa Francis ahimiza maelewano ya kidini Mongolia
3 Septemba 2023Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa mwito wa maelewano katika mkutano wa imani tofauti za kidini wakati wa ziara yake nchini Mongolia.
Papa Francis amesema dini ndio haswa ina dhima ya kuleta maelewano katika ulimwengu uliosambaratishwa na migogoro na mafarakano. Kiongozi huyo alihudhuria mkutano uliowakutanisha wawakilishi kutoka dini tofauti nje kidogo ya mji mkuu wa Mongolia wa Ulaanbaatar.
Papa Francis aionya Mongolia kuhusu rushwa na uharibifu wa mazingira
Francis aliwasili Mongolia siku ya Ijumaa, akifanya ziara yake ya kwanza ya kipapa katika taifa hilo la Asia lililo katikati mwa mataifa mawili makubwa ya Urusi na China. Kiongozi huyo anatarajiwa kufanya misa mchana wa leo itakayohudhuriwa na watu wapatao elfu 2,000 mjini Ulaanbaatar.
Sambamba na Wakatoliki wa Mongolia, mahujaji kutoka China watashiriki misa ya leo. Papa Francis atasalia nchini humo hadi kesho Jumatatu kabla ya kurejea Vatican.