Mabaraza ya maaskofu: Wanawake kuruhusiwa kupiga kura
27 Aprili 2023Kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wanaendesha kampeni ya kuwania haki ya kupiga kura kwenye mabaraza hayo. Mabaraza hayo yalianzishwa miaka 50 iliyopita kwa lengo la kuratibisha mikutano ya maaskofu kutoka duniani kote.
Mpaka sasa ni wanaume tu waliokuwa wanaruhusiwa kupiga kura juu ya mapendekezo yanayowasilishwa kwenye vikao vya maaskofu na pia kwenye baraza la ushauri la baba mtakatifu.
Soma pia: Papa Francis: Madai ya wanawake ni halali kutaka haki zaidi
Wanawake watano watashiriki kwenye mkutano utakaofanyika mjini Rome mnamo mwezi wa Oktoba. Papa Francsia pia ameamua kwamba wajumbe 70, kutoka makundi mbalimbali ya imani, ambao si maaskofu watateuliwa kuwa wajumbe wa baraza la maaskofu.
Nusu yao watakuwa wanawake na watakuwa na haki ya kupiga kura.