1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yaiomba Belarus kuwafukuza Wagner

28 Agosti 2023

Poland na mataifa ya Baltiki yameiomba Minsk kuwafukuza wapiganaji wa kundi la Wagner kutoka Urusi walioingia nchini Belarus baada ya jaribio la uasi lililoongozwa na kundi hilo dhidi ya Moscow mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4Vf78
Russland Flugzeugabsturz l Ermittler bestätigen Tod von Wagnerchef Prigoschogin
Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Poland, Mariusz Kaminski, alisema kwamba azma yao ni kuyalinda mataifa yao dhidi ya kitisho chochote cha usalama.

"Kutokana na hili tunakutana Warsaw kujadili hali kwa kuzingatia mataifa yetu, na kwa pamoja kuangazia hatua za kuchukua ili kuzuia vitisho dhidi ya raia na vitisho kutoka mashariki. Na tutaelezea azma yetu na nia yetu ya kuchukua hatua, ili maeneo yetu yawe salama, ili raia wetu wawe salama." Alisema Kaminski siku ya Jumatatu (Agosti 28), baada ya mkutano na wenzake wa Lithuania, Latvia na Estonia.

Soma zaidi: Vipimo vya DNA vyathibitisha kifo cha Prigozhin
Serikali ya Urusi hatimaye imethibitisha kifo cha Prigozhin baada ya uvumi wa siku kadhaa

Poland inasema maelfu ya wapiganaji wa Wagner wako Belarus inayopakana na Urusi, Ukraine na Poland.

Kulingana na Kaminski, baadhi yao ni wahalifu walioachiwa kwenye magereza ya Urusi kwa ahadi ya kupigana katika vita huko Ukraine. 

Rais Alexander Lukashenko wa Belarus hivi karibuni alisema angeliwabakisha wapiganaji wapatao 10,000 wa kundi hilo nchini mwake.

Hata hivyo, kauli hiyo aliitowa kabla ya kufariki dunia kwa kiongozi wa kundi hilo, Yevgeniy Prigozhin, wiki iliyopita.