Polisi Bangladesh watoa amri mpya ya kutotoka nje
20 Julai 2024Polisi nchini Bangladesh imeweka sheria kali ya kutotoka nje nchini humo huku vikosi vya kijeshi vikishika doria katika sehemu za mji mkuu wa nchi hiyo mapema hii leo ili kutuliza ghasia baada ya siku kadhaa za maandamano ya wanafunzi ya kupinga mgao wa ajira serikalini.
Soma zaidi. Waandamanaji Bangladesh wavamia gereza na kuwaachia wafungwa
Amri hiyo ya kutotoka nje na marufuku ya mikusanyiko ya watu inafuatia baada ya siku mbaya zaidi za maandamano yaliyopelekea vifo vya zaidi ya watu 100 na mamia ya wengine kujeruhiwa. Miili 23 ya watu waliopoteza maisha imeshuhudiwa ikitapakaa katika Chuo cha Matibabu na hospitali mjini Dhaka na haijafahamika wazi kuwa lini watu hao walipoteza maisha.
Maandamano hayo ya wanafunzi yanaangazia nyufa katika utawala na uchumi wa Bangladesh huku wengi wao wakidai kukosa ajira pale wanapohitimu elimu yao.