1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Tanzania yashutumiwa kwa kuhangaisha wanahabari

Hawa Bihoga22 Aprili 2021

Baraza la habari Tanzania limelaani mfululizo wa matukio ya polisi ya kukamata, kushambulia na kuwaweka kizuizini waandishi wa habari nchini humo kwa amri ya baadhi ya viongozi wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

https://p.dw.com/p/3sMYt
Tansania Polizei attackiert einen Journalisten in Dar es Salaam
Picha: Article19-East Africa

Taarifa ya baraza hilo la habari ambalo linatumia kanzi data kuhifadhi matukio inaonesha kwa mwezi April pekee takriban waandishi wa habari watano wamekumbana na unyanyasaji wakiwa katika majukumu yao hatua ambayo inatajwa na wanahabari kuwa hiyo ni ishara mbaya dhidi ya jeshi la polisi na baadhi ya viongozi dhidi ya unyanyasaji huo.

Soma pia: Mkanganyiko juu ya vyombo vya habari vilivyofunguliwa Tanzania

Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni ambalo lilizua mjadala mpana ni pamoja na lile la mkurugenzi wa halmashauri ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, kuwaweka chini ya ulinzi waandishi wa habari wawili walioitwa na wafanyabiashara wa soko la mbagala ambapo walikuwa wakiwasilisha hoja zao kwa mkurugenzi hatua ambayo mkurugenzi huyo aliwaweka chini ya ulinzi hadi pale alipotamatisha mkutano wake kwa madai wamevamia mkutano, tukio ambalo lililaaniwa vikali na wadau wa habari.

Mkuu wa Polisi Tanzania Simon Sirro. (Picha ya maktaba)
Mkuu wa Polisi Tanzania Simon Sirro. (Picha ya maktaba)Picha: DW/S. Khamis

Kajubi mukajanga mkurugenzi mtendaji wa baraza la habari anasema, matukio hayo ya kuwanyanwasa wanahabari wakiwa kwenye majukumu yao wanatafsiri ni kama uvunjifu wa haki za binadamu Kadhalika ni kudhoofisha kada hiyo ambayo imekuwa nyenzo muhimu katika kuunganisha umma na mamalaka.

Soma pia: Vyombo vya habari Tanzania vyatakiwa kupinga rushwa ya ngono

Aidha katibu huyo ameongeza kuwa, tukio la Aprili 9 2021, la mkuu wa wilaya ya nyamagana dokta Philis Nyimbi kumtishia kumfanyia kitu kibaya mwandishi wa ITV Mabere Makubi ambacho kitamsababisha afutwe kazi hii ni kutokana na kutoridhishwa na habari alioitoa, ni sehemu ya unyanyasaji wanaopitia waandishi dhidi ya baadhi ya viongozi wasio thamani mchango wa tasnia hiyo.

Kauli ya rais Tanzania juu ya kufunguliwa vyombo vya habari yazua gumzo lakini pia ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali wa mahesabu yawaamsha waliolala

Baadhi ya waandishi wa habari wanasema, ingawaje haya yanajiri ndani ya siku 15 tangu Rais Samia Suluhu kutangaza Uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari, wanaona bado nafasi ipo ya wote waliohusika kuja hadharani na kueleza sababu za kufanya unyanyasaji huo Kadhalika kuweka maridhiano ili kazi ziendelee bila kuketa hofu kwa wananchi.

Wakati haya yanawekwa hadharani tasnia ya habari Tanzania inatoneshwa donda ndugu la kupotea kwa mwandishi wa habari wa mwananchi Azori Gwanda ambae hajulikani alipo hadi hivi sasa huku mamalaka ikikosa jibu na bado jumuia za kimataifa zikiendelea kutaja kuwa hilo ni doa dhidi ya uhuru wa habari, mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kufikishwa mahakamani kwa tubuma za ukwepaji kodi hatua ambayo ilizua minadala mipana kwenye vyumba vya habari huku wengine wakitafsiri ni kuzorotesha habari za uchunguzi nchini.