1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani yasema wahamiaji haramu waongezeka 2023

21 Agosti 2024

Ofisi ya Polisi ya Shirikisho ya Kupambana na Uhalifu nchini Ujerumani, BKA, imesema idadi ya watu wanaoshukiwa kuhamia Ujerumani kinyume cha sheria imeongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4jjKX
Ujerumani | Mkutano wa BKA huko Wiesbaden
Picha iliyopigwa wakati wa mkutano wa BKA Ofisi ya Polisi ya Jinai ya Shirikisho la Ujerumani (BKA) huko huko Wiesbaden.Picha: Arne Dedert/dpa/picture alliance

BKA imesema leo kuwa polisi inawashuku watu 266,224 kwa kuingia na kusihi bila kibali mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4, ikilinganishwa na mwaka 2022. Wengi wa washukiwa hao walikamatwa na polisi wa shirikisho la Ujerumani. Kulingana na BKA, kwa ujumla, Shirika la Mipaka la Ulaya na Walinzi wa Pwani, limerekodi takribani watu 380,200 waliovuka mpaka bila idhini kwenye eneo la Schengen ambalo hauhitaji visa kusafiria, ikiwemo Ujerumani.