SiasaMarekani
Putin kujibu mpango wa Marekani wa kupeleka silaha Ujerumani
28 Julai 2024Matangazo
Akiongea wakati wa gwaride la wanamaji huko St Petersburg, Putin aliapa kuchukuwa hatua hiyo baada ya Marekani mapema mwezi huu kutangaza kuwa itaanza kupeleka silaha hizo Ujerumani katika mwaka 2026, ili kuthibitisha kujitolea kwake kwa jumuiya ya kujihami ya NATO na ulinzi wa Ulaya kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022.
Soma pia: Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Urusi wajadiliana kupunguza hatari ya kusambaa mvutano
Putin amesema ikiwa Marekani itatekeleza mpango huo, Urusi itajichukulia kuwa huru kutoka kwa usitishaji wa awali wa pande moja wa kupelekwa kwa
silaha za mashambulizi za masafa ya kati na mafupi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa vikosi vya pwani vya jeshi lake la wanamaji.