1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia waandamana Niger kutaka Ufaransa iondoe wanajeshi wake

3 Septemba 2023

Maelfu ya raia wa Niger, jana waliandamana katika mji mkuu wa Niamey kushinikiza kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa. Waandamanaji hao walikusanyika karibu na kambi ya askari wa Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4VtdS
Niger Demo Anti Frankreich
Picha: AFP

Raia hao waliandamana kufuatia wito wa maandamano uliotolewa na mashirika ya kiraia kupinga uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa katika taifa hilo la Afrika Magharibi

Waandamanaji hao walibeba mabango yenye ujumbe wa kulitaka jeshi la Ufaransa kuondoka nchini humo.

Soma zaidi: Niger yajiandaa na maandamano makubwa ya kuipinga Ufaransa

Utawala mpya wa kijeshi wa Niger ulitoa matamshi ya kuishutumu Ufaransa siku ya Ijumaa kwamba inaingilia mambo yake ya ndani kwa kumuunga mkono rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum.

Utawala huo pia umemfukuza balozi wa Ufaransa mjini Niamey Sylvain Itte na kutangaza kumwondolea kinga ya kidiplomasia. Lakini Rais Emmanuel Macron alisifu kazi ya balozi wake siku ya Jumatatu akisema kuwa bado anasalia nchini humo licha ya kupewa masa 48 ya kuondoka.