Rais Assad wa Syria akutana na Kiongozi Mkuu Iran Khamenei
30 Mei 2024Ikulu ya Syria imesema katika mazungumzo ya viongozi hao wawili yaliyohudhuriwa pia na rais wa mpito wa Iran Mohammad Mokhber, Assad na Khamenei wamesisitiza kwamba usuhuba kati ya nchi hizo washirika bado ni madhubuti.
Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa Iran imesalia kuwa muungaji mkono pekee wa utawala wa Assad ulionusurika kuangushwa wakati wa wimbi la mapinduzi ya umma katika ulimwengu wa kiarabu mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Soma pia:Iran yasema Saudi Arabia imewafukuza waandishi habari 6 wa televisheni ya taifa ya Iran
Safari ya Assad mjini Tehran imefanyika katika siku ambayo mamlaka za Iran zimefungua pazia la usajili wagombea wanaotaka kuwania nafasi ya Urais kurithi ile iliyoachwa na hayati Ebrahim Raisi. Usajili utafanyika kwa siku tano na kufuatia na zoezi la mchujo wagombea kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 28.