SiasaUfaransa
Rais Emmanuel Macron kulihutubia taifa Jumatano
21 Machi 2023Matangazo
Hotuba yake itarushwa na vituo mbali mbali vya televisheni nchini humo kesho mchana. Watu chungunzima walikamatwa kote nchini humo kufuatia maandamano yaliyozuka saa chache baada ya serikali kunusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo bungeni jana Jumatatu.
Hatua ya bunge imempa afueni rais Macron na serikali yake kuendeleza mageuzi yake ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 mpaka 64.
Soma pia: Serikali ya Ufaransa yanusurika chupuchupu kura za kutokuwa na imani bungeni
Wabunge wa Upinzani wameapa kushinikiza kuzuia hatua hiyo na vyama vya wafanyakazi vinajiadaa kuchukua hatua ya maandamano ya nchi nzima mnamo siku ya alhamisi.