Rais Macron wa Ufaransa akataa ombi la Waziri Mkuu kujiuzulu
8 Julai 2024Attal alitanagza dhamira ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kufuatia matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge, ambao haujatoa mshindi wa moja kwa moja atakayelidhibiti Bunge la Ufaransa.
Hata hivyo kwenye uchaguzi huo wa jana muungano wa siasa za mrengo wa kushoto wa New Popular Front (NPF) ndio umepata idadi kubwa ya viti kulivyo vyama vingine.
Muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto washinda duru ya pili ya uchaguzi Ufaransa
Kufuatia matokeo hayo Attal anayetoka upande wa rais Macro alitangaza mpango wa kujiuzulu lakini akasema atasalia mamlakani ikiwa itahitajika. Kuondoka kwake kungeiacha Ufaransa bila kiongozi wa serikali ikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki mjini Paris.
Urusi imesema haina matumaini yoyote ya kuimarika kwa mahusiano yake na Ufaransa kufuatia ushindi huu wa muungano wa mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa Bunge.