1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Chad amjibu kebehi rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

7 Januari 2025

Rais Emmanuel Macron amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa washirika wa Ufaransa waliosalia Afrika kufuatia kauli yake ya kutatanisha.

https://p.dw.com/p/4oul2
Rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno na Emmanuel Macron
Rais wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno na Emmanuel MacronPicha: Benoit Tessier/REUTERS

Rais wa Chad  Mahamat Idris Deby amemwambia rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba yuko katika enzi isiyomfaa, baada ya rais huyo wa Ufaransa kusema mataifa ya Afrika yalisahau kulishukuru  jeshi la nchi hiyo lililopelekwa katika kanda ya Sahel kukabiliana na uasi wa makundi ya itikadi kali.

Rais Deby amemjibu Macro kupitia hotuba aliyoitowa ikulu na kuchapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Facebook,  kwa kumwambia kwamba anaishi kwenye enzi nyingine asiyoijuwa.

Soma pia: Ivory Coast yawataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka

Ufaransa hivi sasa inahangaika kutafuta namna ya kuendelea kubakisha uwepo wa jeshi lake barani Afrika baada ya kutimuliwa Mali, BurkinaFaso na Niger. Senegal na Ivory Coast pia zimeitaka nchi hiyo iondowe wanajeshi wake katika mataifa hayo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW